Nenda kwa yaliyomo

Maumivu ya rektamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maumivu ya rektamu
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuUpasuaji wa jumla
VisababishiKawaida: Mpasuko wa njia ya haja kubwa, bawasiri, fistula ya njia ya haja kubwa, jipu la njia ya haja kubwa[1]
Si kawaida: Prostatitisi (Prostatitis), saratani ya njia ya haja kubwa, magonjwa ya zinaa, kuwashwa matumboni, maumivu ya kifandugu, maumivu ya eneo la rektumu[1]
Idadi ya utokeaji wakeKawaida[1]

Maumivu ya rektamu ni dalili za kawaida za eneo la rektamu.[1] Maumivu hayo yanaweza kuongezeka kwa harakati ya matumbo.[1] Dalili zinazohusiana nao zinaweza kujumuisha kutokwa na damu kwenye rektumu, kuwashwa kwa mara kwa mara kwenye njia ya haja kubwa, au homa.[1]

Sababu zake za kawaida ni pamoja na mpasuko wa njia ya haja kubwa, bawasiri zenye mvilio, fistula ya njia ya haja kubwa, na jipu la njia ya haja kubwa.[1] Sababu zake chache za kawaida ni pamoja na prostatitisi (prostatitis), saratani ya njia ya haja kubwa, magonjwa ya zinaa, ugonjwa wa kuwashwa matumboni, maumivu ya sehemu ya chini zaidi ya uti wa mgongo, na kuumwa katika eneo la rektumu.[1]

Kumuona mhudumu wa afya kunapendekezwa kwa wale ambao wana maumivu makali, au ikiwa maumivu yatadumu zaidi ya siku chache, au ikiwa kuna damu.[1]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Anal pain". nhs.uk (kwa Kiingereza). 17 Oktoba 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)